Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. MUHARAMI SHABAN MKENGE, amekutana na kikundi cha utalii cha UTALII KIROMO GROUP ili kufahamu changamoto na mipango ya kikundi hicho katika kuendeleza na kukuza utalii wa vivutio vilivyomo katika wilaya ya Bagamoyo na Tanzania kwa ujumla.
Mhe. Mbunge amewataka wanakikundi hao kuhakikisha wanakamilisha taratibu zote za usajili wa kikundi lakini pia na kuhamasisha wananchi na watalii kufika katika vituo vyetu vya utalii ikiwemo magofu ya kale na mbuga za wanyama.
Huku akipata chakula cha mchana na wanakikundi hao, Mheshimiwa Mbunge amesema kuwa wilaya ya Bagamoyo ina vivutio vingi ambavyo vinaweza kusaidia katika kuongeza pato la taifa litakalo wanufaisha wananchi. na kuwa anautambua mchango wa vikundi vya utalii katika hamasa ya kutangaza vivutio vya kitalii vilivyomo ndani ya nchi yetu.
0 Maoni