Ticker

6/recent/ticker-posts

UZINDUZI WA BAGAMOYO ARDHI CLINIC


NA. Iddi Nassoro Rajabu

Katika uzinduzi wa Bagamoyo Ardhi Clinic uliofanyika leo tarehe 23/09/2023 katika Viwanja vya shule ya msingi Mtambani kata ya Mapinga, jimbo la Bagamoyo. Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo. Maharami Shabani Mkenge alipata wasaa wa kushiriki na kumpongeza Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo. Mhe. Halima Okash kwa kuanzisha programu ya  Bagamoyo Ardhi Clinic ambayo itakuwa ni muarobaini wa changamoto za ardhi katika wilaya ya Bagamoyo. 

katika uzinduzi huo wa Bagamoyo Ardhi Clinic Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Bagamoyo mbele ya waziri wa ardhi maendeleo na Makazi mhe. Jerry silaa aliweka wazi kuwa migogoro mingi ya ardhi katika wilaya ya Bagamoyo inasababishwa na matapeli, viongozi kutokuwa waaminifu na wanasheria kushiriki kudhulumu wananchi ardhi.


Aidha, Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Bagamoyo. Mheshimiwa Muharami Shabani Mkenge alimuomba Waziri wa Ardhi maendeleo na makazi kushughulikia swala la eneo la razaba lenye ukubwa wa Hekta 28,000 ambazo Hekta 12000 zinamilikiwa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Hekta 6,000 zinamilikiwa na Serikali ya  Mapinduzi ya zanzibar na Hekta 10,000 amepewa mwekezaji Bakhressa. ambapo katika hekta hizo alizopewa Mwekezaji kulikuwa na wananchi waliokutwa na Mwekezaji walipatiwa fidia na wote waliondoka katika eneo hilo. 

ila wananchi waliokuwa wakiishi katika eneo lenye ukubwa wa Hekta 12000 ambalo linamilikiwa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wamefanyiwa tathmini na wamepatiwa karatasi zao za fidia lakini mpaka sasa Hawajapatiwa fidia na eneo hilo wamepatiwa TFS kwaajili ya kulisimamia wakati wananchi hawajalipwa bado. Mwisho Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo alimuomba Mheshimiwa waziri wa ardhi kuwasadia wananchi hao wapatiwe fidia zao kama walivyopatiwa fidia wenzao.


Chapisha Maoni

0 Maoni