Mwandishi : Iddi Nassoro Rajabu. March 08/2023
mbunge wa jimbo la Bagamoyo mhe. muharami mkenge siku ya tarehe 08/03/2023 alishiriki katika mahadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kimkoa yalifanyika katika wilaya ya Bagamoyo, kata ya Dunda viwanja vya Mwanakalenge. katika Mahadhimisho hayo ya siku ya wanawake, Mhe. mbunge wa jimbo la Bagamoyo Muharami mkenge alipata nafasi ya kutoa neno katika hafla hiyo na alianza kwa kumshukuru Mhe. Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bi Halima Okash ( muwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa pwani), Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani, Waheshimiwa Wenyeviti wote wa Halmashauri za Mkoa wa pwani, Waheshimiwa wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa wa pwani, Waheshimiwa madiwani wote, Viongozi wa dini, wageni waalikwa na wote waliohudhuria katika Mahadhimisho hayo.
Sambamba na hilo Mhe. Mbunge wa jimbo la Bagamoyo alitoa shukrani zake za dhati kwa kupata fursa ya kufanikisha jambo hilo katika jimbo lake na wilaya ya Bagamoyo kwa ujumla, kwani kwa siku hizo mbili za mahadhimisho ya siku ya wanawake wafanya biashara na wajasiriamali wadogo wadogo wa watafaidika na fursa hiyo.
Katika hotuba yake mhe. mbunge wa jimbo la bagamoyo pia aliwataka wakina mama kuwa karibu na watoto wao ili kuwakinga na vitendo vichafu vya ukatili wa kijinsia na ubakaji kwa watoto kwa kuweka taratibu za kuwakinga kibaiolojia na kisaikolojia.
Mwisho, Mbunge wa jimbo la Bagamoyo alimshukuru Mhe. Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bi Halima Okash (Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa pwani), viongozi meza kuu na watu wote waliohudhuria katika Hafla ya Mahadhimisho hayo.
Tukio picha. Kikosi cha jeshi la Polisi Tanzania kikiongoza Maandamano katika Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo tarehe 08/03/2023
0 Maoni