Katika muendelezo wa vikao vya bunge vinavyoendelea jijini Dodoma, Tarehe 09/11/23 Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Muharami Shabani Mkenge alipata wasaa wa kuwaalika Bungeni Walimu wa Shule ya Bagamoyo sekondari walioambatana na DMO ambaye pia nia Mwenyekiti wa Bodi ya shule ikiwa ni Baada ya Shule hiyo kufanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha sita iliyofanyika miezi kadhaa iliyopita.
Aidha, Katika ziara hiyo iliyofanyika Bungeni Dodoma. Pia Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo alipata wasaa wa kufanya kikao kifupi na Walimu hao ikiwa ni lengo la kuwapongeza na kuwashukuru kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuhakikisha ufaulu unaongezeka katika shule hiyo.
Sambamba na hilo Mheshimiwa mbunge alipata wasaa wa kuwakutanisha walimu hao na Waziri mwenye dhamana ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa Prof. Mkenda ambapo waliweza kuzungumza masuala mbalimbali ambayo yakifanyiwa kazi itasaidia kuboresha na kukuza ufaulu katika shule hiyo.
0 Maoni