Naibu Waziri Mhe. Ummy NdeliYananga akiwa katika ziara hiyo, aliambatana na Mhe. mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Mkurungenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo pamoja na Wataalamu wa Halmashauri kwenda kukagua sehemu iliyotengwa kwaajili ya kujengwa mradi mbalimbali ikiwemo
1. Ujenzi wa vichanja vya kukaushia samaki kwa njia ya jua (Dry racks),
2. Ufungaji wa Mahema ya Kukaushia Dagaa (Solar tents),
3. Mradi wa uwekaji wa vivutia samaki baharini FADs (Fish Aggregative Devices),
4. Mradi wa Ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha barafu ( Ice plant),
5. Kukamilisha ujenzi wa soko la samaki pamoja na
6. Mradi wa kusambaza mbegu za samaki kwa Wafugaji wa samaki.
Mpia, Mhe. Naibu waziri Ummy NdeliYananga alipata fursa ya kutembelea soko la samaki pamoja na kukagua shughuli mbalimbali zinazoendelea katika soko hilo.
0 Maoni