Ticker

6/recent/ticker-posts

VETA KUJENGWA BAGAMOYO





Mwandishi: Iddi Nassoro Rajabu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akizungumza wakati alipotembelea Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan itajenga vyuo vya VETA katika kila wilaya nchini.

Waziri, Prof. Mkenda aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika ziara aliyoifanya Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo, ambapo alisema Rais Samia tayari ameilekeza Wizara ya Elimu kuwa, kila wilaya iwe na chuo cha VETA.

Alisema tayari wizara ya elimu imejipanga kutekeleza maelekezo ya Rais samia ya kujenga chuo cha VETA kila wilaya ambapo wilaya zote 64 zitajengwa kwa mkupuo pamoja na kimoja kitakachojengwa mkoani Sngwe.

Prof Adolf Mkenda, aliyasema hayo kufuatia ombi la Mbunge wa Bagamoyo, Muharam Mkenge aliyemuomba Waziri huyo wa Elimu kujenga chuo cha VETA katika jimbo la Bagamoyo ili vijana wa Bagamoyo waweze kujifunza fani mbalimbali katika chuo hicho.

Mkenge alisema kwa sasa Bagamoyo inakuwa kwa kasi katika uwekezaji wa viwanda na kutoa fursa mbalimbali kwa vijana wazawa wenye ujuzi wa fani mbalimbali na kuongeza kuwa fursa hizo hazitakuwa na faida kwa vijana wa Bagamoyo ikiwa hawatakuwa na ujuzi wa fani yoyote.

Aliongeza kwa kusema kuwa kwa sasa kuna ushindani mkubwa katika soko la ajira hivyo uwepo wa chuo cha VETA chenye kutoa ujuzi wa aina mbalimbali kutasaidia kwaa vijana wa Bagamoyo kukabiliana na ushindani katika soko la ajira na kufaidika na uwekezaji unaofanyika katika jimbo hilo.

Alisema tayari mchakato wa kupata eneo la kujenga chuo hicho kwa Bagamoyo umeshakamilika na kupata eneo lenye ukubwa ekari 38 ambzo zitatumika kujenga chuo cha VETA.

Aidha, Mbunge Muharam Mkenge alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuelekeza fedha za elimu katika jimbo la Bagamoyo hali iliyopelekea kuanzishwa kwa shule mpya za sekondari ambazo zimesaidia kuwapungzia watoto kwenda umbali mrefu kufika shuleni.




Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, akizungumza mbele ya Waziri wa Elimu, katika Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) kilichopo mjini Bagamoyo.

Katika hotuba yake mbele ya mgeni rasmi, Mhe. mbunge wa jimbo la bagamoyo Muharami Mkenge, ali,shukuru Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hasani kwa kuleta miradi mingi ya Elimu katika kipindi kifupi.

Mhe. Mbunge wa jimbo la bagamoyo alimueleza Mhe. Waziri Prof. Adolf Mkenda kuwa ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wa Mama Samia Suluhu Hassani Bagamoyo imebahatika kupata shule 3 za sekondari ambazo ni Udindivu mapinga, Shule ya sekondari Nianjema na Shule ya Sekondari makurunge katika kata ya Makurunge.

Pia Mhe. Mbunge wa jimbo la bagamoyo, Muharami mkenge  alizungumzia juu ya kupatikana kwa shule nne (4) shikizi, Katika kata ya Mapinga, Kerege, Fukayosi na Yombo. 

Mwisho, Mhe. Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Muharami mkenge alimuomba Mhe. waziri kufanya mchakato wa haraka ili Chuo Cha veta kijengwe katika jimbo la bagamoyo, Kwani kwa sasa kunauhitaji mkubwa kutokana na uwekezaji mkubwa wa viwanda unaofanyika ili vijana wetu waweze kupata ujuzi ili waendane na kasi ya viwanda.



 
Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Utawala wa ADEM, Dkt. Emanuel Molel, wa pili kulia ni Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu, Bw. Manori Venance, na watatu kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ADEM, Dkt. Naomi Katunzi, kutoka kushoto wa kwanza ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, wapili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib Okash, na watatu kushoto ni Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Siston Mas.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib, akizungumza katika Ukumbi wa Chuo cha ADEM Wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipotembelea chuoni hapo jana February 17, 2023.


Mtendaji Mkuu wa 
Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akizungumza katika Ukumbi wa Chuo hicho Wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipotembelea chuoni hapo jana February 17, 2023.




Viongozi wa Elimu Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo, Watumishi wa Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa pamoja wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, alipokuwa akizungumza wakati alipotembelea chuo cha ADEM Bagamoyo jana Februry 17, 2023.


Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja, akimkabidhi Waziri wa Elimu, Taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya ADEM na machapisho mbalimbali yanayo onesha kazi za ADEM kwa ujumla.



Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri- ADEM, Dkt. Naomi Katunzi (kulia) akimkabidhi zawadi ya T-shirt za ADEM, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kushoto)


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kulia) akijaribu zawadi ya T-shirt aliyopewa na uongozi wa ADEM, Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kulia) akimkabidhi zawadi ya T-shirt, 
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Halima Habib, anaeshuhudia (katika) ni Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Siston Masanja.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, (kulia) akimkabidhi zawadi ya T-shirt, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, (kushoto).




Picha ya pamoja ya Mhe. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Mbunge wa Jimbo la bagamoyo, Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Uongozi wa chuo cha Adem bagamoyo pamoja na Watumishi wa Chuo hicho.




Chapisha Maoni

0 Maoni