Ticker

6/recent/ticker-posts

MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA BAGAMOYO WAENDELEA NA ZIARA YA MAFUNZO GEITA MJI.

 

Watembelea mradi wa Zahati ya Nyamkumbi iliyojengwa Kwa mapato ya ndani, wafurahishwa na Biashara Soko la Dhahabu linamilikiwa na Halmashauri ya Mji wa Geita


Wahemiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo tarehe 4 Disemba 2023 wameendelea na ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Mji Geita Kwa kukutana na Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita ukiongozwa na Mkurugenzi wa Mji wa Geita Bi Zahara Michuzi katika ukumbi wa mikutano.




Mkurugenzi huyo aliwakaribisha wajumbe Toka Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Mohamed Usinga.  Akitoa taarifa ya Miradi ya Maendeleo pamoja na ukusanyaji wa mapato Bi Zahara Michuzi alisema kuwa, Uchumi na mapato ya Halmashauri ya Mji Geita inategemea sana Kodi za machimbo ya Dhahabu."Nieseme tuu Kwa asilimia kubwa mapato yetu yanategemea machimbo ya dhahaba pamoja kilimo kidogo" . Alisema Bi Michuzi.









Chapisha Maoni

0 Maoni