Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, MUHARAMI SHABAN MKENGE leo tarehe 06/01/2024 ametembelea kikundi cha CHAMBEZI GROUP kilichoanzishwa mwaka 2006 ambacho kina jumla ya wanachama 69 kilichoundwa na muunganiko wa Vijiji vinne ambavyo ni Kijiji cha Buma, Matibwa, Mataya pamoja na Kiromo, kwa lengo la kusikiliza kero zinazokikabili kikundi hicho.
Katika kikao hicho cha CHAMBEZI GROUP Mheshimiwa Mbunge amewataka wanakikundi kuendelea kufikiria biashara mbadala itakayowasaidia kuongeza kipato cha kikundi kwani baadhi ya biashara nyengine zina changamoto hasa katika uendeshaji. mhe. mbunge ameyasema haya mara baada ya kikundi hicho kuwasilisha lengo la kupata basi aina ya Coasta kwaajili ya kusafirisha abilia.
Aidha, Wanakikundi hao waligusia juu ya changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara na walimuomba Mhe. Mbunge wa jimbo la Bagamoyo kuwatafutia wafadhili na wadau kuweza kuwasaidi kutatua kero hiyo.
Akijibu kuhusu suala la barabara. Mhe. SALUMU MIKUGO, Diwani wa kata ya kiromo amewaambia wananchi wa vijiji vya Buma na Kiromo kuwa changamoto ni kuwa Barabara zetu hazijasajiliwa hivyo hazitambuliwi na Serikali na mpaka sasa yeye na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo wanaendelea na mpango wa kuhakikisha usajili wa Barabara unafanyiwa kazi iliziweze kutambulika na Serikali iliiwe rahisi kwa barabara hizo kuingia katika mpango wa kutengezwa ikiwemo Barabara inayounanisha kata ya YOMBO na KIROMO yenye kilomita 11.9
Mwisho, Mhe. MUHARAMI SHABAN MKENGE ametolea ufafanuzi kuhusu suala la mikopo ya vijana inayotolewa na halmashauri, swali lililoulizwa na mwanakikundi Kivumbi Muhamedi. kuwa atalifuatilia suala hilo kwa Mkurugenzi wa halmashauri ilikujua taratibu na namna ya ukopaji kwa mikopo hiyo kwa vijana. na kuwahasa wananchi wanaochukua mikopo hiyo kuwa waaminifu na kuirudisha mikopo hiyo ndani ya muda wa makubaliano ili fedha hizo ziweze kuwanufaisha pia na wengine.
0 Maoni