Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri mkuu ya CCM Mkoa wa Pwani Mhe. Mubarami Shabani Mkenge Leo May 11/ 2024 Alikuwa Mgeni Rasmi katika Kikao cha Mkutano Mkuu wa CCM Tawi la Mwambao uliofanyika katika Ofisi ya CCM ya Tawi hilo.
Kupitia kikao hicho Mhe. Muharami Mkenge alipokea taarifa ya kazi iliyoambatana na changamoto mbalimbali zikiwemo uchakavu wa jengo la ofisi ya CCm tawi hilo la Mwambao, Changamoto ya Mafuriko kwa baadhi ya Wananchi, Changamoyo ya wamiliki wa Magofu kuto ya fanyia usafi Magofu yao, Msamaa wa kodi ya matibabu kwa wazee, Changamoto ya kukatika katika kwa umeme mara kwa mara imekuwa kero kwa wananchi pamoja na Changamoto ya Mfereji unao toka kwa Mzungu kuelekea Zakaria haujamaliziwa hivyo imekuwa kero na ni hatarishi katika eneo hilo kwani inapelekea kuharibu miundombinu ya eneo hilo.
Mhe. Mkenge Baada ya kupokea Taarifa hiyo na kuzungumza aliweza kutolea ufafanuzi wa kero hizo kama ifuatavyo :-
- uchakavu wa jengo la ofisi ya CCm tawi hilo la Mwambao, Changamoto hii aliipokea pia aliahidi kuifanyika kazi changamoto hiyo kwani taarifa ya uchakavu wa jengo hilo alipatiwa mapema na alishamtuma mtu wa Tathimini hivyo anasubili kupatiwa bajeti ya ukarabati wa jengo hilo kisha atafanya mchakato wa kutafuta namna ya kufanikisha ukarabati huo.
- Changamoyo ya wamiliki wa Magofu kuto ya fanyia usafi Magofu yao, Moshi unaotokana na kuchomwa kwa takataka hatarishi katika Hosp[itali ya wilaya ya Bagamoyo imekuwa kero, Katika changamoto hii Mhe. Mbunge wa jimbo la Bagamoyo aliomba kupatiwa ushirikiano wa kuwapata wamilikiwa magofu hayo kwani asilimia kubwa ya magofu hayo yanamilikiwa na watu Binafsi hivyo alikuwa anaomba ushirikiano wa kuwapata wamilikihao ili aweze kuzungumza nao,.
- Moshi unaotokana na kuchomwa kwa takataka hatarishi katika Hosp[itali ya wilaya ya Bagamoyo imekuwa kero, Changamoto hiyo aliahidi kuifikisha kwa ( DMO) ili iweze kufanyiwa kazi.
- Msamaa wa kodi ya matibabu kwa wazee, Swala la kodi kwa wazee, Mhe. mbunge alilitolea ufafanuzi kuwa lipo katika mchakato wa Serikali kupitia Wizara yake ya Afya ambapo mchakato wa kuwafanyia Sensa wazee unaendelea baada ya kukamilika wazee wote watahakikishiwa wanapatiwa bima ya Afya ili iweze kuwasaidia katika matibabu yao.
- Changamoto ya kukatika katika kwa umeme mara kwa mara imekuwa kero kwa wananchi Changamoto hii mhe. Mbunge aliitolea ufafanuzi ya kuwa, kuhusu swala la umeme kwa sasa unatokana na uchakavu wa miundombinu kwani swala la Mgao wa umeme kwa sasa limesha kwisha kilichobaki ni maboresho ya miundo mbinu ya Umeme hivyo tuwe wavumilivu katika kipindi hiki cha Maboresho.
- Changamoto ya Mfereji unao toka kwa Mzungu kuelekea Zakaria haujamaliziwa hivyo imekuwa kero na ni hatarishi katika eneo hilo kwani inapelekea kuharibu miundombinu ya eneo hilo. Changamoti hii alitoa ahadi kuwa atatenga siku na atakujana Mhandisi wa Tarura kuja kuona namna ya kutatua changamoto hiyo.
- Changamoto ya Mafuriko kwa baadhi ya Wananchi wa Eneo hilo, Kupitia kikao hicho mhe. alitoa ahadi ya kutenge siku kwaajili ya kuwapapole wahanga hao na kuona namna ya kuwezesha kuboresha miundombinu ya eneo hilo.
Mwisho , Baada ya kumaliza kutoa Maelezo juu ya kero hizo alitoa shukrani zake za dhati kwa Kamati ya siasa ya Tawi la Mwambao kwa kuona kuwa yeye anafaa kuwa mgeni Rasmi wa kikao hicho na kuhitimisha kwa kuwaasa kukisimamia chama Pamoja na jumuiya zake ili kiweze kuwa imara kwa upande wa tawi na aliahidi kuwa bega kwa benga wa kati wote watakapo muhitaji.
0 Maoni