Mheshimiwa Mbunge ametembelea makazi ya wananchi wa kata ya mapinga kitongoji cha Kihalaka mtaa wa Minazi Minane walioathiriwa na maji ya mvua iliyosababisha baadhi ya maeneo kutoweza kupitika wa urahisi na kuharibu makazi yao.
akiwa kwenye eneo yaliyoathiriwa na maji, Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Mhe. MUHARAMI SHABAN MKENGE ameahidi kufuatilia kwa karibu kwa namna gani wataweza kufanya maboresha ya Barabara hasa mitaro ambayo imekuwa kilio cha wananchi wengi wa kitongoji chicho.
Ndugu SIMON JOSEPH KILIAN mwenyekiti wa kitongoji cha kihalaka ameiomba serikali kupitia kwa mheshimiwa Mbunge kuwa itengeneze mitaro iliiweze kupunguza kiwango cha maji kutuaama na kuharibu mali za wananchi.
0 Maoni